The House of Favourite Newspapers

BEKA FLAVOUR Atamani Kumfugia Mpenzi Wake Mbwa

Bakari Katuti ‘Beka Flavour’

MWANA-MUZIKI ambaye alikuwa ni memba Yamoto Band kabla ya kusambaratika, Bakari Katuti ‘Beka Flavour’ amefunguka kuwa anatamani sana hata kumfugia mbwa mpenzi wake Sophia, kila anapoenda.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Beka alisema kuwa, amekuwa na mapenzi makubwa sana kwa mpenzi wake huyo kiasi ambacho anatamani kumuwekea ulinzi wa mbwa kila mitaa anayokatiza.

 

“Mapenzi niliyonayo kwa Sophia wangu ni makubwa mno, natamani sana ningeweza kumlinda popote anapoenda awe na mbwa ili asisogelewe na mtu yeyote yule kwa sababu nampenda sana jamani,” alisema Beka ambaye hata hivyo hana mpango wa kumuoa msichana huyo kwa sasa japokuwa anampenda hadi atakapoweka mambo yake sawa.

IMELDA MTEMA

Comments are closed.