The House of Favourite Newspapers

Bella Amshukuru Rais Samia kwa Kuukubali Muziki Wake na Kumpongeza Jijini Dodoma

0
BELLA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpongeza Msanii Christian Bella kwenye uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma  tarehe 06 Aprili, 2022.

Christian Bella au King Of The Best Melodies; ni staa wa muziki wa Dansi nchini Tanzania ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuukubali muziki wake na kumpongeza.

 

Tukio hilo lilijiri juzi Jumatano kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura kwa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-MAMA).

 

Halfa hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ambapo Bella alishusha zile melodi zake hasa za wimbo wa Nani Kama Mama na kukonga nyoyo za wengi akiwemo Rais Samia ambaye alimfuata na kumpongeza.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA juu ya kitendo hicho, Bella anasema; “Mtu mwingine anaweza kuona ni jambo dogo, lakini kwangu ni tuzo kubwa sana kwa Rais kutambua kazi yako. Mimi nasema asante President na namuombea atomize majukumu yake vizuri kwa sababu Watanzania wanampenda,”

Stori; Mwandishi Wetu, Dodoma

SOKO LA KURUME (ILALA) LATEKETEA TENA, TAZAMA HALI ILIVYO, WAFANYABIASHARA WAANGUA VILIO

Leave A Reply