The House of Favourite Newspapers

BENJAMIN MKAPA AKABIDHI CHETI CHA SHUKRANI NMB KWA UDHAMINI MAONESHO NANENANE SIMIYU

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , Benjamin Mkapa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa NMB Bank, Ineke Bussemaker ikiwa ni shukrani kwa udhamini wa Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. NMB ilikuwa mmoja wa wadhamini wakuu wa maonesho hayo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenesta Mhagama (kulia) akimkabidhi Meneja Uhusiano Mwandamizi idara ya Kilimo biashara wa benki ya NMB, Oscar Rwechungura kombe la ushindi wa kwanza taasisi za fedha kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo Kanda ya Kaskazini Nanenane Themi mkoa wa Arusha, kushoto ni Meneja Uhusiano Biashara za serikali,Christabel Hiza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenesta Mhagama (kulia) akiwakabidhi Meneja Uhusiano Biashara za serikali wa benki ya NMB, Christabel Hiza(kushoto) na Meneja Uhusiano Mwandamizi idara ya Kilimo biashara,Oscar Rwechungura kombe la ushindi wa kwanza taasisi za fedha kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo Kanda ya Kaskazini Nanenane Themi mkoa wa Arusha.

 

Comments are closed.