The House of Favourite Newspapers

Benki Ya NMB Kupokea Maoni Ya Wateja Wake

nmb-2-001Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

nmb-3-001…Akizungumza jambo na Meneja wa Kanda Mkoa wa Dar,Vicky Bishubo (katikati) na Meneja Huduma NMB Tawi la Msasani, Helen Mapunda.

nmb-4-001Mmoja wa wafanyakazi wa tawi hilo, Godliver Mwendo (kulia) akipokea cheti baada ya kuonekana kwa kipindi cha mwezi moja kuwazidi wafanyakazi wenzake kutoa huduma bora kwa wateja.

nmb-5-001Bussemaker (kushoto) akisalimiana na RPC Mkoa wa Kinondoni, Salome Kaganda, aliyehudhuria hafla hiyo.

nmb-6-001Baadhi ya wafanyakazi wa NMB Tawi la Masasani wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo.

BENKI ya NMB leo imewashauri wateja wake kutumia mwezi huu kufikisha mapendekezo na maoni yao mbalimbali juu ya kuboresha huduma zao za kibenki.

Hayo yamesemwa katika tawi la NMB Msasani jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker,  katika hafla fupi ya kuadhimisha wiki na mwezi wa huduma kwa wateja ambapo siku hiyo huadhimishwa kila mwaka.

“Ninapenda wateja wetu muelewe kuwa wiki ya kwanza ya mwezi wa kumi ni wiki ya huduma kwa wateja kila mwaka ambapo sisi  kwetu ni siku ya huduma kwa wateja hivyo nawaomba wateja wetu watumie fursa hii kuleta mapendekezo na maoni mbalimbali ili na sisi tuweze kuyafanyia kazi katika kuboresha  huduma zetu katika matawi nchi nzima,” alisemaBussemaker

Alifafanua kuwa katika kufanikisha malengo ya serekali ya awamu ya tano ya kujenga na kuendeleza viwanda , benki hiyo imejipanga vyema kuhakikisha inafanikiwa katika malengo hayo.

Mbali na kueleza malengo yao pia wateja waliweza kupata huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo kuuliza maswali kwa watendaji wa benki hiyo ili kupata huduma bora na kuelezea matatizo yao.

“Katika huduma zetu zipo huduma tunajitahidi kufanya vizuri na kuna huduma zinaweza kuwa na matatizo, hatuwezi kusema tupo sahihi kwa aslimia mia moja, lakini kwa maoni na ushauri wenu kwetu tunaweza kuboresha huduma zetu na kufanya NMB kuwa benki bora zaidi,” alisema Meneja wa Kanda Mkoa wa Dar,Vicky Bishubo.

Naye Meneja Mkuu wa Shirika la Viwanda na Tafiti (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Mtambo ameipongeza benki hiyo kwa hatua zake mbalimbali za kusaidia katika kukuza na kuboresha viwanda nchini na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo.

NA DENIS MTIMA/GPL.

Comments are closed.