The House of Favourite Newspapers

Beyonce Hubadili E-mail Kila Wiki!

Staa wa Pop kutoka Uingereza Ed Sheeran amefichua siri ya mkali wa R&B, Beyonce.

MSANII wa Pop kutoka Uingereza Ed Sheeran amefichua siri ya mkali wa R&B, Beyonce kuwa kumpata kwake ni vigumu na kwamba kila wiki hubadili e-mail kukwepa usumbufu. Akizungumza na Entertainment Tonight, Ed Sheeran ambaye amefanikiwa kufanya kolabo moja ya Perfect Remix akiwa na Beyonce alisema, haikuwa rahisi kumpata mara moja.

 

“Nakumbuka mara ya kwanza wakati nataka kufanya naye kolabo nilimtumia e-mail ikawa pending tu ndio nilipoamua kufanya mawasiliano kwa njia ya simu, lakini kolabo yetu ilikamilika mwezi Septemba,” alisema Ed Sheeran. Ukiachana na Beyonce, msanii mwingine ambaye kuwasiliana naye sio rahisi kabisa ni Kanye West.

LONDON, Uingereza

Comments are closed.