‘BILIONEA’ WA MAJUMBA YA LUGUMI AJIDHAMINI

Aliyekuwa anajulikanakama bilionea mwenye kununua nyumba za Lugumi kwenye mnada, Lous Shika.

ALIYEKUWA anajulikanakama bilionea mwenye kununua nyumba za Lugumi kwenye mnada, Lous Shika, ameachiwa na jeshila polisi lililokuwa linamshikilia kwa tuhuma za kuvuruga mnada wa nyumba hizo wikiiliyopita.

 

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amethibitisha  hilo leo mbele ya waandishi wa habari leo ambapo Shika amejiwekea dhamana mwenyewe na atakuwa anaripoti polisi kufuatana na masharti aliyopewa.

 

Mambosasa alifafanua zaidi akisema uchunguzi wa anachotuhumiwa Shika unaendelea na amejidhamini mwenyewe kwani hakuna mtu aliyejitokeza kumdhamini.

 

Aliendelea kusema mtu huyo ambaye anajulikana kama Dk. Shika aliyeshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa uuzaji wa majumba ya kifahari ya Saidi Lugumi, ameachiliwa baada ya ufuatiliaji mkubwa wa watu kuhusianana suala hilo.

 

Kwa mujibu wake, alisema aliwaagiza maofisa wa chini yake wamwachie Shika kutokana na kutoeleweka makazi yake.

Shika  amekuwa maarufu nchini tangu wiki iliyopita wakati wa mnada huo kwa kushiriki kwake katika mnada wa ununuzi wa majumba hayo akiwa anapandisha bei kwa mamilioni ya shilingi lakini hatimaye akagundulika kwamba hakuna na fedha yoyote ya kutanguliza kama kithibitisho cha dhamira ya kununua nyumba hizo.

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment