The House of Favourite Newspapers

BILL NAS ASHINDWA KUPATA MBADALA WA NANDY

Tokeo la picha la bill nass
William Lyimo ‘Bill Nas’

HITMAKER wa Ngoma ya Labda, William Lyimo ‘Bill Nas’ amefunguka kwamba anatamani sana kuwa kwenye uhusiano lakini kinachomfanya mpaka sasa kuwa ‘single’ ni kwamba hafahamu mwanamke yupi ni sahihi kwake.

Akipiga stori na Star Showbiz, Bill Nas ambaye aliwahi kuwa katika uhusiano na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ alifunguka kwamba hahitaji kukurupuka, anachotamani ni kupata mtu sahihi ili aweze hata kufunga naye ndoa na si kuwa kwenye uhusiano ambao unaanza leo na kumalizika kesho.

“Watu wanaweza wasiamini lakini ukweli ni kwamba kwa sasa sina uhusiano wa aina yoyote ile. Kinachonikwamisha kuingia ni kwamba sioni bado mwanamke sahihi wa mimi kuwa naye. “Ninasubiri pengine Mungu anionyeshe, huyo nitakayempata ndiye atakuwa mke wangu na sihitaji uhusiano wa kuanza leo na kuvunjika kesho,” alisema Bill Nas.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.