The House of Favourite Newspapers

Binti Alia: Shemeji Kanilewesha, Kanibaka!

ARUSHA: Binti mwenye umri wa miaka 14 (jina tunalihifadhi), mkazi wa Njiro Kwa Msola Katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, amelazwa Katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru akidai kubakwa na shemeji yake aliyemtaja kwa jina la Yusufu baada ya kuleweshwa na kileo kinachodaiwa kuchanganywa na dawa za kulevya.

 

Akiongea kwa uchungu huku akitokwa machozi, binti huyo alidai kuwa kutokana na tukio hilo, amejikuta akitolewa ‘usichana’ alioutunza kwa muda mrefu.

“Unajua dada alisafiri kwenda Ghana akamwomba huyu shemeji (Yusuf) awe anakuja kutujulia hali, lakini badala yake alitumia nafasi hiyo kunibaka,” alisema binti huyo. Aidha, aliongeza kuwa kitendo hicho kimemfedhehesha na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri ambapo amedai kushindwa hata kukaa kutokana na maumivu makali anayoyapata.

 

“Siku ya tukio huyu shemeji alikuja na chupa ya wine akanilazimisha kunywa, nilikuwa sijawahi kutumia kileo chochote tangu nizaliwe, nilikunywa kidogo kidogo na baada ya muda nikawa sijitambui, nadhani alitumia nafasi hiyo kunifanyia tukio hilo,” alidai binti huyo.

 

Akizidi kusimulia tukio hilo, alisema kuwa, kesho yake alipoamka alishangaa kuona damu zikiwa zimetapakaa kitandani na alikuwa akisikia maumivu makali sehemu za siri. Hata hivyo, baadaye aliwaeleza majirani ambao waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi Themi kilichopo eneo hilo.

 

Alidai kuwa hakuweza kupata msaada katika kituo hicho ambapo kesho yake Aprili 14, mwaka huu, alienda kituo kikuu cha polisi cha mjini kati na kupatiwa hati ya matibabu PF3 kisha kwenda kulazwa Katika Hospitali ya Mount Meru baada ya polisi kumfungulia jalada la kunajisi lenye kumbukumbu namba, AR/ RB/4559/2018. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusufu Ilembo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema bado wanamsaka mtuhumiwa.

Stori: Joseph Ngilisho.

Comments are closed.