The House of Favourite Newspapers

BLAC CHYNA: SINA UJAUZITO, NIMENENEPA TU

 

 

MWANAMITINDO  maarufu wa Marekani, Blac Chyna, amesema hana ujauzito kama mashabiki wake wanavyoeneza, hususani kutokana na kufutuka kwa tumbo lake ambapo amewaambia hiyo inatokana na kuongezeka tu kwa unene wake.

 

Chyna ambaye jina lake halisi ni Angela Renée White, aliyekuwa amehudhuria mahafali ya mwanaye kwenye kituo cha chekechea cha King, aliwafanya watu waliofika hapo wahisi ana ‘kitumbo’ kutokana na nguo yake ya pinki aliyokuwa amevaa kumbana.

Chyna amekuwa akionekana kila mara na rafiki yake wa kiume, YBN Almighty Jay, hivyo watu wanafikiri tayari ‘amenasa’.  Msanii huyo tayari ana watoto wawili kutoka kwa mabwana zake  wa awali ambao ni  Tyga na Rob Kardashian.

 

 

Comments are closed.