The House of Favourite Newspapers

BOKO HARAMU YAKANUSHA KUSAMBARATISHWA NA SERIKALI

KUNDI la wapiganaji la Boko Haram la Nigeria, limekanusha kauli ya serikali ya Nigeria kwamba limesambaratishwa na majeshi ya serikali.

Hilo limesemwa na kiongozi wa kikundi hicho, Abubakar Shekau,  aliyeonekana katika mkanda mpya wa video siku moja baada ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, kutangaza hadharani kuwa kikundi hicho kimesambaratishwa.

Shekau amesema  kundi lake ndilo limekuwa likihusika katika matukio nchini humo hususan  maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo  yakiwemo yale ya  sikukuu ya Krismasi katika kijiji cha Molai, mji mkuu wa Jimbo la Borno.

Kiongozi huyo wa Boko Haram amesema askari wake wako katika afya njema na kwamba vikosi vya ulinzi nchini Nigeria haviwezi kuwafanya lolote  wanamgambo hao aliosema wako imara siku zote.

Pia ametoa tamko la kulaani nchi zilizoutambua  mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israeli ambapo Rais wa Marekani Donald Trump ameutambua uamuzi huo wa Israel.

 

 

 

WALUSANGA NDAKI na MITANDAO/BBC

Comments are closed.