The House of Favourite Newspapers

BREAKING: KILOMONI AKAMATWA NA POLISI… AACHIWA – VIDEO

Polisi wakiongea na Hamisi Kilomoni nyumbani kwake Block 41 Kinondoni jijini Dar es Salaam.

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Simba, Hamisi Kilomoni, leo Alhamisi Julai 25, 2019, ameachiwa na polisi jijini Dar es Salaam baada ya kukamatwa na kutakiwa kuandika barua ya kuomba ruhusa ya kufanya mkutano na wanahabari.

“Wao wameniambia nimekatazwa, na kwamba lazima nikaombe kibali cha kufanya mkutano,” alisema Kilomoni alipohojiwa na vyombo vya habari.

Kilomoni akipanda gari ya polisi.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo, alikamatwa na polisi  wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Block 41 Kinondoni,  na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Oyster Bay jijini Dar kwa mahojiano.

Polisi hao wamesimamisha mkutano huo wakitaka kufahamu endapo alikuwa amepata kibali cha kufanya mkutano huo.

Hilo lilitokea muda mfupi kabla ya kukaribishwa ili aanze kuelezea sababu aliyowaitia waandishi wa habari.

Wanahabari wakiwa eneo la tukio. 

Katika mwendelezo wa tukio hilo, Kilomoni alipotakiwa kupanda kwenye gari aligoma na kuwaeleza polisi kwamba asingeweza kupanda gari na kukaa nyuma bali alitaka kukaa mbele kando ya dereva, jambo ambalo baada ya ubishi, polisi  walikubali akae mbele.

Hata hivyo, alichokuwa anakataa Kilomoni kupanda nyuma ni kutokana na kusumbuliwa na miguu ambapo hawezi kuinyanyua kiurahisi.

Comments are closed.