The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Chuo Kikuu Akutwa Akikodisha Bastola, Dar – Video

0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza a wanahabari.

JESHI la Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam linamshikilia Robson Isack Maji (22) ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na baba yake mzazi kwa kukamatwa na bastola aina ya Beretta na risasi sita.

Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa kijana huyo alikamatwa Septemba 20 majira ya saa 2:30 usiku  maeneo ya Mwenge, Dar akiwa katika harakati za kutaka kuikodisha bastola hiyo.

“Siku ya tukio, askari walipata taarifa na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea. Alikamatwa akiwa na bastola aina ya Berreta yenye namba DAA316502 ikiwa na risasi sita ndani ya magazine.

“Mwanafunzi huyo alikuwa akitaka kukodisha silaha hiyo kwa majambazi kwa gharama ya Tsh. 400,000 lakini pia alikuwa tayari kuiuza kwa Tsh. Milioni 2,500,00.

“Kwa mahojiano ya awali na mtuhumiwa huyo ilibainika kuwa silaha hiyo aliiba kwa baba yake aitwaye Isack Maji ambaye naye siye mmiliki halali wa silaha hiyo. Kwa hiyo, baba na mtoto wote tunawashikilia na tunaendelea kuwahoji watuambie waliitoa wapi sambamba na kumpata mmiliki wa silaha hiyo” alisema Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema jeshi hilo likiwa doria, limekata gari la wizi lenye namba za usasjili T 364 DJV, aina ya Noah nyeupe katika maeneo ya Mbezi jilani na St. Joseph University kilichopo Mbezi jijini hapa.

Mbali na hayo, katika oparesheni zake, jeshi hilo limekamata wauzaji wa pombe haramu ya gongo, mitambo ya kuchemshia pombe hiyo, bangi na kete za madawa ya kulevya ambapo watuhumiwa wote bado wanaendelea kuhojiwa na polisi.

SHUHUDIA TUKIO HILO.

Leave A Reply