The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: EDWARD LOWASSA AREJEA RASMI CCM – VIDEO

ALIYEWAHI kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amerejea rasmi kwenye chama chake cha awali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chadema na kupokelewa na Rais John Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally leo Ijumaa, Machi 1, 2019 katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zangu kama alivyozungumza Lowassa ametumia maneno mafupi, amerudi nyumbani na nyumbani ni hapa CCM, ndio maana amesimama kwenye jengo la Makao Makuu Ofisi ndogo ya CCM” amesema Rais Magufuli wakati akimpokea Lowassa.

Mwaka 2015, Lowassa ambaye alikuwa Mbunge wa Monduli, alihama CCM na kujiunga Chadema baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mchakato wa kuwania Urasi, alipojiunga na Chadema aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya kuwania Urasi akichuana na Magufuli aliyekuwa CCM lakini Lowassa alishindwa.

Wakati Lowassa akihamia CCM leo alikuwepo pia rafiki yake wa muda mrefu, Rostam Aziz ambaye miezi michache alikwenda Ikulu kuzungumza na Rasi Magufuli baada ya kutoonekana kwa muda mrefu.

 

Lowassa alishaonekana mara kadhaa akikutana na Rais Dokta John Magufuli na kufanya naye mazungumzo katika Ikulu ya Tanzania huku Umma ukiwa haufahamu chochote kuhusu mazungumzo yao, Hatua ambayo ilizua minong’ono kuwa ana mipango ya kurudi CCM.

 

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, kumekuwa na wimbi la wapinzani kuhamia CCM, hatua ambayo imeelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa upinzani unadhoofika.

Comments are closed.