The House of Favourite Newspapers

Brown Mauzo: Wakenya wengi wanajua mi ni Mtanzania

global-tv-8Msanii wa Kenya, Brown Mauzo akiwa katika pozi kabla ya kufanyiwa mahojiano.

global-tv-7Brown Mauzo mara baada ya kufanyiwa mahojiano.

MKALI wa Muziki kutoka Kenya, Fredrick Mutinda ‘Brown Mauzo’ ameweka wazi kuwa kabla ya kutoka kimuziki Wakenya wengi walikuwa wakimuona na kumsikia tofauti na kudhani huenda ni Mtanzania.

Akizungumza na Global TV Online kupitia kipindi cha Mtu Kati, Brown Mauzo anayetikisa kwa sasa na Ngoma ya Nitulize alioshirikiana na Ali Kiba pia alizima tetesi zilizokuwa zikizagaa kuwa alikuwa na bifu na Ali Kiba kisa kikiwa ni kumgomea kufanya naye kolabo.

brown-mauzo-1Brown Mauzo.

“Hizo maneno ndiyo kwanza nazisikia huku TZ, Kiba ninavyomjua ni mtu poa sana. Uongozi wangu na wake ulikutana na kufanya naye mazungumzo ya kolabo akakubali na kusema kuwa nina kipaji kikubwa sana,” alisema Brown Mauzo.

Brown Mauzo ambaye awali alikuwa akiishi Mombasa kwa sasa amehamishia makazi yake jijini Nairobi. Aliwahi kufanya kolabo Bongo na mastaa kibao wakiwemo, Rich Mavoko na Bob Junior.

Kwa mahojiano zaidi na kumuona Brown Mauzo jinsi alivyofunguka mengi, tutembelee katika mtandao wetu wa www.globaltvtz.com

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Comments are closed.