The House of Favourite Newspapers

Wakazi wa Bukoba Walala Nje ya Nyumba Baada ya Tetemeko Kutokea Mara ya Pili

BUKOBA: September 10, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi Kagera kanda ya ziwa Tanzania lenye kipimo cha ritcha 5.7 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa ambapo ndani ya saa 24 baadae (September 11 saa tano kasoro usiku) likatokea tena tetemeko jingine na kuacha tahauki kwa wakazi wa Bukoba.
Tetemeko hilo la pili ambalo ni dogo halijaripotiwa kusababisha majeruhi au vifo mpaka usiku wa saa nane lakini limeleta hofu kwa wakazi wa Bukoba ambao baadhi wameamua kutoa magodoro nje ya nyumba zao na kulala kwa kuhofia tetemeko linaweza kutokea tena usiku na kuwakuta ndani ya nyumba zao.
 
 

Comments are closed.