The House of Favourite Newspapers
gunners X

Bwana Harusi Afanya Sherehe Mwenyewe Baada Ya Bibi Harusi Kugomea Harusi – Video

0
Edward Futakamba Mkazi wa Kata ya Nsemlwa

Bwana Edward Futakamba Mkazi wa Kata ya Nsemlwa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amejikuta kwenye sintofahamu baada ya aliyekuwa mke wake mtarajiwa, Mary Mbogo kugoma kufunga ndoa na bwana huyo.

Wakiwa ukumbini, Ndugu wa Bwana harusi na wageni waliochangia michango ya harusi hiyo, bwana harusi hakuwa na namna badala yake alimua kufanya sherehe ya harusi katika ukumbi licha ya Bibi harusi kugoma kufunga ndoa hiyo.

 

Edward amekuwa akiishi na Mary Mbogo kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu(3) kabla ya kuamua kufunga ndoa.

Familia za wawili hao zilikubaliana na kutoa mahali ya shilingi 1,200,000/- na mwanaume kutoa kiasi cha shilingi Mil. 1,000,000 na maandalizi ya harusi kufanyika ili ndoa ifungwe Julai 26, 2024.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya harusi hiyo Simon Moshi amesema siku nne kabla ya harusi walipata taarifa kutoka upande wa Bibi harusi kuwa wameweka pingamizi kanisani la kuzuia ndoa hiyo.

Leave A Reply