The House of Favourite Newspapers

CALISAH AJITAPA KWA UFUSKA!

Image result for calisah
Calisah Abdulhamid

MWANAMITINDO asiyeishiwa skendo mjini, Calisah Abdulhamid amefunguka kwa mara nyingine tena kuwa katika ukuaji wake mpaka sasa alipofikia ameshatembea na wanawake wapatao elfu moja, kwa sababu ilifika kipindi kila siku alikuwa akitembea nao watatu. Calisah aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, kabla hajawa staa alishatembea na wanawake kama wengi na baada ya kuwa staa akatembea na wengine zaidi na hii yote inatokea kwa sababu asilimia kubwa ya wanawake walikuwa wanajipeleka wenyewe.

“Waache kujirahisisha na waamini kwamba wanaweza kuwatengeneza wanaume wao wenyewe, waache tamaa kuna watu wananitamani na wanataka kuwa na mimi kimapenzi kwa sababu nina jina, navutia, lakini hawajui kama kuna mtu alimtengeneza Calisah tangu yupo chini au kuna kipindi nakosa kabisa pesa, lakini kuna mtu ananielewa na maisha yanasonga mbele, hivyo nawasihi dada zangu wajiamini,” alisema Calisah.

Comments are closed.