The House of Favourite Newspapers

CALISAH APATA ZALI MR AFRIKA 2018

Calisah Abdulhamiid

Mwana-mitindo anayezidi kuja kwa kasi Bongo, Calisah Abdulhamiid, amepata zali la kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya kushiriki Shindano la Mr Africa International, ambalo linachukua mtu mmoja toka Afrika na kumpeleka nchini humo.  Akizungumza na Star Showbiz, Mwanamitindo huyo alisema kwamba, imekuwa ni furaha kubwa sana kwake kualikwa kwenda nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mr Afrika, hivyo anaimani kubwa kuwa atafanya vizuri na Tanzania itakuwa namba moja na ndiyo maana sasa hivi anafanya sana mazoezi.

“Nilitumiwa barua mwaka jana ya kwenda kushiriki Mr Africa International, lakini nilishindwa kwenda kwa sababu kwanza nilichelewa kupata barua yao halafu pia nilitakiwa kujilipia tiketi ya ndege mwenyewe kwenda na kujilipia hoteli kwa siku kadhaa ambazo ningekuwepo huko.

“Lakini kwa bahati nzuri tena mwaka huu wamenitumia tena mwaliko, kwa hiyo natakiwa kwenda Nigeria mwezi wa 10 kwa ajili ya hayo mashindano na mimi ndiyo Mtanzania pekee ambaye nimechaguliwa kwenda na ninajua kabisa nitashinda,” alisema Calisah

Comments are closed.