David Cameron .
Theresa May leo anakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke katika historia ya nchi ya Uingereza baada ya Margaret Thatcher aliyetumikia nafasi hiyo kati ya 1979-1990. Waziri mkuu huyo mtarajiwa huenda akaongeza nafasi nyingi zaidi za wanawake kwenye baraza la mawaziri. Mwanamama Amber Rudd huenda akateuliwa katika moja ya nafasi nyeti ya waziri wa mambo ya ndani au waziri wa fedha.
Justine Greening.
Justine Greening na Priti Patel waliokuwa vinara wa kutaka nchi ya Uingereza kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya wanapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na waziri mkuu mpya anayeamini umefika wakati wa wanawake kupewa majukumu zaidi katika nafasi nyeti ndani ya serikali.
Priti Patel.
Waziri mkuu mtarajiwa anaweza kuvunja rekodi ya kuwateua wanawake wanane kwenye baraza lake la mawaziri.
Leo asubuhi waziri mkuu aliyejiuzulu atawasilisha barua kwa Malkia Queen Elizabeth II itayohitimisha utawala wake na kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya ya May.