The House of Favourite Newspapers

Chadema Wakanusha Lissu Kuerejea Nchini

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene amesema; Kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba Lissu anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia juzi na kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho si cha kweli na kimezua taharuki.
Makene amesema, Lissu hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote kuhusu kurejea kwake hapa chini kwa sababuĀ  hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwishoni wiki hii au wiki ijayo.
Chadema kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo.
Lissu yupo nchini Ubelgiji akipatiwa awamu ya tatu ya matibabu baada ya kumaliza matibabu nchini Kenya mwezi Januari ambapo alikuwepo huko kwa takribani miezi minne ambapo alikuwa akiuguza majeraha ya risasiĀ zaidi ya 30 alizopigwa nyumbani kwake Dodoma, Septemba 7, mwaka jana.

Comments are closed.