The House of Favourite Newspapers

Chan Yaanza Leo Bila Stars

Wallace Karia.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, ameteuliwa na Caf, kuwa kamishina wa mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) kati ya Morocco na Mauritania.

 

Michuano ya Chan ambayo inaanza leo Jumamosi huko Casablanca, Morocco, mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya wenyeji Morocco dhidi ya Mauritania. Taifa Stars haitashiriki Chan kwavile haikufuzu baada ya kutolewa na Rwanda.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, alisema; “Mchezo huo ambao Rais Karia atausimamia kama kamishna, utachezwa kwenye uwanja wa nyasi asilia wa Mohamed V, Casablanca.”

 

Alisema hivi karibuni Karia aliteuliwa na Caf kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ya Chan itakayomalizika Februari 4, mwaka huu.

 

Kwa ukanda wa Cecafa, nchi zilizofuzu kucheza Chan ni Sudan, Rwanda na Uganda. Uganda itacheza kesho Jumapili na Zambia wakati Rwanda itacheza keshokutwa na Nigeria. Sudan inacheza kesho na Guinea

Comments are closed.