The House of Favourite Newspapers

Chanzo ni Saa, Mwalimu Ampa Mimba Mwanafunzi wa Miaka 15

0

WAZAZI na wa mwanafunzi wa kike (15) aliyekuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kolero wilayani Morogoro (jina limehifadhiwa), wamelilalamikia jeshi la polisi kushindwa kumchukulia hatua mwalimu anayetuhumiwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo huku akiendelea kutamba kijijini hapo.

 

Akizungumzia namna tukio hilo lilivyotokea mwanafunzi huyo amesema kuwa chanzo cha hayo yote ni mwalimu kuchukua saa ya mwanafunzi huyo na kisha baadaye alimuomba urafiki na kuanza kumletea zawadi kidogo kidogo na ndipo mazoea yao yalipozidi.

 

Akisimulia zaidi mwanafunzi huyo amesema, mwalimu huyo alimuahidi kwamba angemsaidia katika masomo yake na kwamba angemuoa ila baada tu ya kumpa ujauzito hajawahi kumsaidia kwa chochote.

Leave A Reply