The House of Favourite Newspapers

Chaz Baba kutimkia Ughaibuni

0

Stori: Musa Mateja
BAADA ya kuutumikia Muziki wa Bongo Fleva kwa muda mrefu, mkongwe Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ ametangaza kuibuka na bendi itakayofahamika kwa jina la QS International.
ALIYEKUWA Prezidaa wa Mashujaa Music Band, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, anatarajia kwenda nchini Oman kwa ajili ya mapumziko mafupi ambapo akirejea ataanza maisha mapya katika bendi mpya.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Chaz Baba alisema mpango wake kwa sasa ni kuangalia mambo mengine nje ya Mashujaa, hivyo kabla hajaanza maisha mapya atakwenda nchini Oman kwa ajili ya mapumziko na baada ya kurejea nchini ataangalia bendi gani mpya ya kuitumikia.
“Kwa sasa mimi siyo rais tena wa Mashujaa Band nipo pale kama wanamuziki wengine wa kawaida kwani majukumu hayo amepewa mtu mwingine (Fagason) kwa kile walichodai wakurugenzi wangu kuwa mimi ni msumbufu hivyo wameona sifa za kuiongoza bendi hiyo zimepungua.
“Nitakwenda Oman kwa mapumziko na baada ya kurejea nitaangalia wapi nitatua kwa ajili ya maisha mapya ya muziki, naomba nisitafsirike vibaya ila nieleweke tu kwamba nina plani za kupumzika kazi hizi na kufanya mambo mengine kisha nitajua wapi nikite nanga,” alisema.

Leave A Reply