Chegge amsapoti Sanjay Boy
MKALI kutoka TMK Family, Chegge Chigunda, amefunguka kuwa anaguswa na uwezo wa bwa mdogo anayekuja kwa kasi kwenye gemu, Andrew John ‘Sanjay Boy’.
Chegge alisema anasapoti harakati zake kwani anaamini kwamba Sanjay anayetarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Moyo ni tishio la hapo baadaye.
“Niwaombe mashabiki pia wamuunge mkono, jamaa anaweza, ukisikiliza wimbo wake wa Ng’aring’ari utagundua uwezo wake, namshauri asikate tamaa, akaze buti,” alisema Sanjay Boy.


