The House of Favourite Newspapers

Chemical: Nimetolewa Bikira na Wanaume Wawili

RAPA wa kike wa bongo Chemical ‘mwana wa Lubao’ amefunguka na kudai haikuwa jambo rahisi ya yeye kutolewa usichane wake na mwanaume mmoja kwa kuwa alikuwa amekomaa sana hivyo ikapelekea kutembea na wanaume wawili kwa wakati mmoja katika kutekeleza jambo hilo.

 

Chemical amefunguka hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV na kusisitiza kuwa licha ya kuwa yupo katika mahusiano lakini hana malengo ya aina yeyote kwa kipindi hiki kufunga pingu za maisha ‘ndoa’ mpaka pale atakapojihakikishia yeye mwenyewe ameweza kukamilisha kila alichokuwa anakihitaji kukipata.

 

“Nimekaa hiyo miaka 20 sio midogo, kwa hiyo ikabidi wasaidiane. Yote hayo yamefanyika nikiwa na akili zangu wala sijatumia pombe maana nilipanga kitolewe na kwa kuwa wa kwanza alishindwa ili bidi aje mwingine amalizie kuitoa”, alisema Chemical. 

 

Rapa huyo amedai hawezi kujutia kutokuolewa na mwanaume ambae ametoa usichana wake ‘bikra’ kwa kuwa anawajua wanaume waliokuwa wengi hawana mapenzi ya kweli huwa wanabadilika muda wowote wakijisikia.

 

“Sijasema kama ninaingia kwenye ndoa baada ya miaka mitano au 10, ‘no’ sijasema hivyo. Watu hubadilika sana anaweza mtu akakupenda leo halafu kesho asikupende na kwangu mimi hilo suala nipo fresh kabisa kwa hiyo sijaingia katika mahusiano kwa kusema huyo ndio atakuja kunioa leo wala kesho”, alisisitiza Chemical.

CREDIT: EATV

Comments are closed.