The House of Favourite Newspapers

CHIRWA, MHILU WAONGEZEWA MBINU KUWAUA WAETHIOPIA

YANGA ni kama tayari imeshafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya bechi la ufundi la timu hiyo, kuiboresha safu ya ushambuliaji kwa kuwaongezea mbinu mbadala za ushindi katika mechi dhidi ya Wolayta Dicha ya nchini Ethiopia.

 

Yanga jana alfajiri ilisafiri kuelekea nchini humo kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Jumatano saa kumi kamili jioni kwa saa za Tanzania.

Katika msafara huo, wachezaji wote wamesafiri huku akikosekana kipa, Ramadhani Kabwili, Maka Edward, Said Mussa walio kwenye kikosi cha vijana wa timu ya taifa ya U20 na Ibrahim Ajibu mwenye majeraha.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Msaid­izi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema tayari wamefanyia marekebi­sho kwenye safu ya ushambuliaji ambayo ilisababisha washindwe kupata mabao mengi katika mchezo uliopita jijini Dar es Salaam.

 

Nsajigwa alisema, safu hiyo ya ushambuliaji tayari wameiimarisha ili kuhakikisha wanai­tumia vema kila nafasi watakay­okuwa wanaipa­ta katika mchezo huo wa marudiano baada ya ku­ona udhaifu wa mabeki wa Dicha.

“Tulicheza na Dicha katika mechi iliyopita ya hapa nyumbani tukiwa hatuwajui vizuri, lakini katika mchezo huu wa marudiano, tutaingia uwanjani tukiwa tunajua udhaifu wao wakiwemo wachezaji hatari.

 

“Katika mechi iliyopita, wache­zaji wetu wakiwemo washam­buliaji, walicheza bila ya kufuata maelekezo yetu na hasa katika kip­indi cha kwanza kwani tuliwaam­bia wacheze mipira mirefu kutokana na mabeki wa Dicha kutokuwa na kasi, lakini tu­kashukuru kipindi cha pili walibadilika na kucheza kwa maelekezo licha ya kushindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga mabao.

“Hivyo, baada ya kuwajua vizuri Dicha tumewaambia viungo wetu akiwemo Tsh­ishimbi (Kabamba), Buswita (Pius) na Daudi (Raphael) ku­wapigia pasi ndefu washam­buliaji wetu ili wakimbizane na mabeki wa Dicha ambao tumewaona ni dhaifu kwani hawana kasi,” alisema Nsajigwa.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.