The House of Favourite Newspapers

 AFYA YA CHOKI YAZIDI KUIMARIKA

Image result for alichoki
Ali Choki

BAADA ya siku chache zilizopita kuwa hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, mapafu na presha, mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ali Choki kwa sasa anafurahi baada ya hali ya afya yake kuzidi kuimarika.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Choki alisema kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo hivyo Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu ataendelea na kazi ya muziki katika bendi anayoitumikia kwa sasa ya Super Kamanyola jijini Mwanza.

 

“Nina furaha kwani kwa sasa naendelea vizuri, hali yangu inaimarika kila siku, Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu nitapanda jukwaani kama kawaida kwa ajili ya kuwapagawisha mashabiki wangu,” alisema Choki.

Comments are closed.