The House of Favourite Newspapers

CHRIS BROWN, RITA ORA SIO SIRI TENA

Image result for chriss brown and rita ora

BAADA ya kukaa kwa muda mrefu bila kumuweka hadharani mwanamke anayetoka naye kimapenzi, mkali wa muziki wa R&B nchini Marekani, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ ameamua kuvunja ukimya kwa kumuanika msanii mwenzake, Rita Ora kama mpenzi wake mpya.

Chombo kimoja cha habari cha MTO NEWS kimethibitisha kuwa, wawili hao ni wapenzi baada ya kuchunguza nyendo zao kwa muda mrefu tangu walipoanza kukomentiana katika kila picha maneno yenye viashiria kuwa kuna mapenzi kati yao.

Chris na Rita walikutwa wakiwa pamoja usiku mzima katika onesho moja la mavazi, Milan huko Italia na kuelekea klabu ya usiku ambapo walikunywa na kucheza na baadaye kwenda kulala pamoja hotelini.

Comments are closed.