MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema, ameitembelea familia ya mwanamama aliyeangukiwa na mti katika kibanda chake cha biashara na kupelekea kifo chake siku mbili zilizopita ambapo chanzo kinatajwa ni mvua ya upepo mkali.
Inatajwa kuwa mwanamama Zulfa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 48, alifariki hapohapo baada kuangukiwa na mti huo, ambapo licha ya mvua hiyo ya upepo kusababisha kifo pia inatajwa kuezua mabati ya baadhi ya nyumba eneo hilo la kata ya Viwege Bomba Mbili.
DC Mjema ametembelea eneo hilo na kutoa pole kwa familia na kuwaambia kuwa serikali ipo pamoja nao.
Comments are closed.