Deal Done: Dube Atua Azam FC
AZAM Football Club ya jijini Dar es Salaam imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube, kutoka Highlanders FC ya huko.
Dube ambaye ni mmoja ya washambuliaji hatari Zimbabwe, akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo cha wachezaji wa ndani, anakuja Azam kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.
Benchi la ufundi la Azam chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, limeridhishwa na uwezo wake kwa muda wote waliomfuatilia hadi kuamua kumsajili.
Huo unakuwa usajili wa saba kwenye kikosi cha Azam katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya msimu ujao. Wengine ni kipa David Kissu, na beki wa kushoto Emmanuel Charles.
Wachezaji wengine walioongezwa ni kiungo mkabaji, Ally Niyonzima, viungo washambuliaji, Awesu Awesu, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.
Zoezi hilo litafungwa karibuni kwa kumsajili mshambuliaji mwingine wa kimataifa.




