Deal Done Zimbwe Aongeza Mkataba Msimbazi
NAHODHA msaidizi wa Simba Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’, leo Aprili 28 ameongeza mkataba wa kuendelea kukipiga kwenye timu hiyo.
Kupitia ukurasa wa Simba kwenye mtandao wa Instagram wamethibitisha beki huyo kuongeza mkataba. Na kuandika- DONE, Contract extension. Bado yupo sana Msimbazi.
Kumwaga wino kwa beki huyo kuna zima tetesi zilikuwepo kuwa anatua Jangwani baada ya mkataba wake kuelekea ukingoni.