The House of Favourite Newspapers

Denti Udsm Alia Miguuni Kwa Shigongo

udsm1-1Watoa mada wakiongozwa na Shigongo katika maombi.

udsm1-2Kijana Haleluya akimuangukia jukwaani.

udsm1-3…Shigogo akimuangalia kijana huyo.

udsm1-5…Akiongea jambo.

udsm1-6Haleluya akizungumza na wanasemina.

udsm1-7Shigongo akizungumza na fundi seremala ambaye ni mlemavu wa macho.

udsm1-8Wajasiriamali wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kusalimiana na watoa mada.

udsm1-9Shigongo akicheza muziki wa Injili na mwimbaji Tumaini Njole.

Na Gabriel Ng’osha/GPL

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anayechukua masomo ya sanaa wa mwaka wa kwanza, Haleluya Kalanje (21), jana aliwashangaza wahudhuriaji wa Semina ya Ukombozi wa Kiuchumi baada ya kumlilia miguuni mwezeshaji na mtoa mada, Eric Shigongo.
Kalanje alifanya hivyo wakati semina ikiendelea ambapo alipanda jukwaani na kuanza kumlilia Shigongo kwa kumkumbatia miguuni kwa uchungu akionesha kuguswa na ushuhuda wa maisha yake.
Katika tukio hilo lililowatoa wengine machozi, Haleluya alionekana ni mwenye huzuni iliyochanganyikana na mawazo. Baada ya Shigongo kubembelezwa kwa muda, hatimaye Haleluya aliomba maiki na kuzungumza: “Nimefurahi kukutana nawe Shigongo, wewe ni kama baba yangu kwa sababu baba yangu mzazi sijawahi kuishi naye. Mama yangu amenifundisha kusoma magazeti yako kwa sababu ni mnunuaji na msomaji mzuri, mama amenilea kwa shida na hata chuo nimefika kwa sababu yake.
“Ninaamini kuonana nawe ni sehemu ya mimi kutimiza ndoto zangu za kucheza sinema baadhi ya hadithi zako ikiwemo ya The President Loves My Wife.’’
Semina hiyo iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya Mikopo ya Wezesha Mzawa Microfinance iliwakutanisha mamia ya wajasiriamali ambao wanakiri kunufaika na semina hiyo.

halotel-strip-1-1

HIVI KWELI KARIAKOO HAKUNA WASOMI?

Comments are closed.