Diamond Amuandikia Manara Waraka Mzito

 

STAA wa Bongofleva nchini, Naseeb Abdul alimaarufu kama ‘Diamond Platnumz’ ameshusha waraka mzito kuelezea ushawishi wa msemaji wa zamani wa klabu ya Simba, Haji Manara ulivyomfanya kupenda na kufuatilia masuala ya mpira wa miguu nchini.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mondi ameandika hivi; “Ukiachana na  Upenzi wangu wa team ya Simba ambao kiukweli umetokana na ushawishi wako… lakini kama Mtanzania ninaependa maendeleo ya tasnia ya michezo, nimeumia kutokuwepo kwako tena simba.

 

“Licha ya kuiongezea Hamasa, ushawishi timu yetu ya Simba, lakini kupitia mbwembwe zako za usemaji, utani kwa Yanga na timu mbalimbali ulifanya tasnia ya michezo kuchangamka zaidi na hata ambao tulikuwa si wafatilia kandanda kuanza kufatilia, kuhudhuria na kwa namna moja au nyingine tasnia ya mpira wa miguu kuongezeka pato zaidi.

 

“Inshallah mwenyezi Mungu ajalie kheri yake siku moja haya yote yaishe na urejee tena kuwa msemaji wa SIMBA…kwasababu kiukweil kwa shabiki wa kweli wa Simba kuondoka kwako lazima  kumuumize, maana thamani ya mchango wako Simba unafahamika…..Inshaallah Mwenyezi Mungu azidi kukufungulia kheri, akulinde na akuepushe na kila baya.”

 

Aidha, Manara ambaye saa chache aliunguruma kuhusu kuondoka kwake Simba, naye akajibu; “ Thanks Mwambaaaaaa tuendelee kuisapot Simba yetu always … diamondplatnumz.”


Toa comment