The House of Favourite Newspapers

Diamond Atuma Ujumbe Mzito Kwa Zari

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond Plutnumz’, akiwa na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’  enzi za mahusiano yao.

 

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond Plutnumz’, usiku wa kuamkia leo amemwandikia mzazi mwenzie,  Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ujumbe mzito katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Diamond amesema ataendelea kumheshimu Zari kwani amemzalia watoto wawili ambapo kwake yeye anaona  ni jambo kubwa sana na zawadi iliyo njema.

“Hii ni siku muhimu sana kwako mama watoto wangu, Nashukuru kwa kunizawadia watoto wawili wazuri sana na kikubwa zaidi umekuwa mama mwema unawalea watoto vizuri.“ amendika Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza hisia zake zaidi.

 

“Niamini mimi, nitaendelea kukuheshimu daima ndio maana hauji kusikia nikikuzungumzia hovyo kwenye interview zangu ninazofanya, sio hivyo tu hata kuzungumzia chanzo cha mfarakano wa mapenzi yetu kamwe siwezi, watoto wetu tuliojaaliwa ni zawadi tosha kwangu,. Nitaendelea kukupenda, kukuheshimu na kukuchukulia kama dada yangu wa damu.“amemaliza Diamond Platnumz.

 

View this post on Instagram

 

A very special Birthday to the Mother of my Beloved kids…Thank you for blessing me with 2 amazing & cute Kids and thank you for continue being a good Mother to my Kids….Trust me, no matter how crazy & a proud man you think i might be, but am always grateful and i do respect you for that…thats why, you’ve never heard or saw me on any interview talking anything about you….not even talking about my side point of what happened to us!!…coz the kids you blessed me with, means alot to me…..and that is what made Love, respect and take you more than a blood sister / Brother for Life!✊🏼….May God bless you with long life, Happiness, and More Winning!!! 🎉🥂🎂🥂🍾🎉

A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Comments are closed.