The House of Favourite Newspapers

Diamond, Bob Junior Wamaliza Bifu Lao, Collabo Mpya Soon – Video

MKALI wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekutana na aliyekuwa producer wake wa ngoma zake mbalimbali tangu kitambo hocho, Bob Junior ikiwa ni miaka kadhaa baada ya kuingia kwenye bifu zito lililowafanya kutenga katika kazi zao.

 

Bob Junior ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na producer wa kwanza aliyerekodi albumu ya kwanza ya Diamond yenye nyimbo kama Kamwambie na Mbagala, baadae waligombana na kukaa bila kuzungumza kwa miaka kadhaa licha ya Diamond kutaka suluhu.

 

Diamond na Bob Junior waliingia kwenye bifu kwa madai ya kugombania jina la Sharobaro huku baadhi ya mashabiki wao wakidai Diamond alimwalika Bob Junior kwenye sherehe yake lakini hakwenda ndipo bifu lao lilipoanza hivyo hakukuwa na sababu ya moja kwa moja iliyotajwa na wasanii hao kwa nini walitofautiana.

 

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Bob Junior ameandika;

SOMTHING BIG ITS COMING 🔥🔥🔥 JAMBO KUBWA MNOO LAJA SINA LAKUSEMA ZAIDI YA APO ONLY HITS ALLOW 🔥🔥🔥🔥🔥SHAROBARO X WASAFI @bobjuniortz X@diamondplatnumz

Edwin Lindege | Global Publishers

Comments are closed.