The House of Favourite Newspapers

Diamond Kujenga Uwanja Tandale, Shigongo Atoa Pikipiki

Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameziagiza mamlaka husika za aradhi jijini hapo kufanya mchakato wa kumpatia ardhi msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa ajili ya kujenga uwanja wa michezo na chuo cha sanaa.

 

Makonda alitoa agizo hilo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika tafrija ya msanii huyo aliy­oifanya mitaa ya Tandale Sokoni katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aliitumia kugawa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Tandale.

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Awali, Diamond alitoa pendek­ezo hilo alipokuwa akihutubia mbele ya umati wa watu ulihud­huria tafrija hiyo ya wazi na ndipo Makonda akaagiza mamlaka ziku­tanane na Diamond ili kufanya mchakato wa kumpatia ardhi kwa lengo hilo mitaa ya Tandale.

 

Staa huyo ambaye sherehe yake ya kuzaliwa rasmi ilikuwa Oktoba 2, 2018 aliamua kuitumia siku hiyo ya jana kutoa misaada Tan­dale kwa kuwa ni eneo ambalo alizaliwa na kukulia.

 

Diamond alitoa bima ya afya kwa watu 1,000 kupitia Kampuni ya Resolution, bo­daboda 20 kwa vijana ambao hawana ajira pamoja, maten­ki manne kwa Shule ya Msingi ya Hekima na mitaji kwa wa­nawake.

Umati wa watu waliofika Uwanja wa Magunia.

Naye, Mkuru­genzi wa Global Group, Eric Shin­gongo ambaye alikuwa mmoja wa wageni alitoa pikipiki tatu na kufanya idadi ya pikipiki zilizotolewa kuwa 23.

 

Akizungumza ali­popewa nafasi, Shigon­go ambaye ndiye mtu wa kwanza kumlipa fedha nyingi Diamond kwa ajili ya shoo, alisema inawezekana vijana wa Tandale kuwa kama Diamond ikiwa wataamua kuji­tuma na kukwepa tabia ovu.

Mkuru­genzi wa Global Group, Eric Shin­gongo.

“Jiepushe na tabia mbaya, ulevi, kila mmoja anaweza kufanikiwa, Tan­zania ni nchi nzuri, hapa kuna mawaziri na rais, mnao uwezo wa kununua nyumba za Masaki,” alisema Shigongo.

 

Baadhi ya wageni maarufu waliohudhuria ni Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta, Rayvanny, Lavalava, Chid Benz, Mboso, Asha Baraka, Katibu wa Basata, Jaque­line Mengi, Haji Manara, Queen Darleen na Mama Diamond.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaam| PICHA: RICHARD BUKOS

Comments are closed.