The House of Favourite Newspapers
gunners X

Dkt. Abbasi Atembelea Makumbusho za Mahatma Gandhi

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye Wizara hiyo kwa Tanzania inasimamia sekta ndogo ya Makumbusho, Dkt. Hassan Abbasi, akiwa nchini India kikazi ametembelea Makumbusho za Baba wa Taifa la India Mzee Mahatma Gandhi “Bapu.”

Makumbusho hizo, ile ya Taifa ya Gandhi na ile ya kwenye nyumba maarufu “Birla House” ambapo aliishi kabla ya kuuawa Januari 30, 1948, zimesheheni kumbukizi mbalimbali za maisha na nyakati za Gandhi na hutembelewa na namilioni ya watalii kwa mwaka kutoka mataifa mbalimbali.

“Moja ya masuala tuliyojifunza hapa ni namna ya kuhifadhi vitu muhimu vinavyowahusu viongozi wetu waliotoa mchango kwa nchi kwani ni ushuhuda wa vizazi vya sasa kujifunza uzalendo na kujitoa kwa waliopita.

“Wenzetu hapa wamemfanya kiongozi huyu abaki kuwa johari ya thamani kitaifa na kimataifa pia ndio maana humu kuna nyaraka na mambo yake mengi aliyoyafanya au anayokumbukwq nayo ikiwemo wamehifadhi hadi stampu zenye picha za Gandhi zilizotumika miaka ya nyuma nchini Tanzania lakini ipo video ya wimbo maarufu aliokuwa anaupenda Mzee Gandhi ambayo imeimbwa upya na wasanii mbalimbali duniani akiwemo Mtanzania Vanessa Mdee na vyote hivi vimetupa cha kujifunza tunapoendelea kuboresha Makumbusho za wazee wetu kama Julius Nyerere na wengine wengi,” alisema Dkt. Abbasi.

Kupitia falsafa yake ya “Satyagraha” Mzee Gandhi alihubiri kusimama katika ukweli, amani, upendo, kuvumiliana, kusameheana na kupendana katika masuala ya siasa na uongozi.

JANUARY MAKAMBA ALIVYOMKABIDHI OFISI BALOZI KOMBO – ”HII KAZI ITABAKI KWENYE MAISHA YANGU”…

Leave A Reply