The House of Favourite Newspapers

DODOMA YAONGOZA KUKUSANYA MAPATO, MBEYA YA MWISHO – VIDEO

 

Jiji la Dodoma limekuwa la kwanza kati ya majiji sita hapa nchini kwa kusanya bilioni 25.5 toka kwenye lengo la kukusanya bilioni 19.3 Sawa na 130% huku Jiji la Mbeya likiwa la mwisho kwa kukusanya bilioni 7 toka kwenye lengo la kukusanya bilioni 10 Sawa na 71%.

 

hayo yameelezwa leo na Waziri wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo na kuzitaka Halmashauri zipatazo 14 nchini ambazo zimekusanya mapato yake chini ya asilimia 50 kujieleza kwa Waziri huyo kwa kutofikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.

 

“Halmashauri zilizofanya vibaya ni halmashauri za Siha, Mbinga, Songea na Rorya, Mikoa iliyofanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato kiujumla ni; 1.Dodoma 130% 2. Geita 104% 3. Njombe 103% na mikoa yote hii imevuka malengo ya makusanyo Mikoa iliyofanya vibaya kwenye ukusanyaji mapato ni 1. Ruvuma kwa 46% 2. Simiyu 59% 3. Shinyanga 66%.

 

“Halmashauri ambazo hazikukusanya hata nusu ya lengo ni; Iringa DC, kyerwa DC, Mbulu DC, kishapu DC, Igunga DC, Itilima DC, Itigi DC, Ubungo, Ilemela, siha, Rorya, Songea DC na mwisho kabisa ni Mbinga DC. Kwa mwaka ujao wa fedha kipimo cha utendaji kazi kwa wakurugenzi kitakuwa ni kasi ya ukusanyaji wa mapato na kufikia malengo ya ukusanyaji huo, na wakurugenzi waanze kujitathimini wenyewe”

 

Pia Waziri Jaffo ameelekeza Halmashauri zote nchini zikusanye mapato juu ya asilimia 81 ili kusaidia uboreshaji na utekelezaji wa miundombinu na kuwaagiza wakuu wa Mikoa kusimamia utekelezaji na matumizi ya makusanyo yaliyopatikana.

 

Katika mkutano huo uliolenga kutoa taarifa za makusanyo ya mapato kwa kila halmashauri na majiji nchini, Waziri Suleiman Jaffo ametaja mikoa iliyofanya vibaya zaidi kwa kukusanya mapato chini ya asilimia 50, ambayo ni Ruvuma, Simiyu na Shinyanga.

UKUSANYAJI wa Mapato Jiji la Mbeya Lashika Mkia

Comments are closed.