The House of Favourite Newspapers

Dongo la Polepole kwa Wapinzani, ‘Muulizeni Mwenyekiti Wenu Alikopeleka Pesa’

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amevipiga kijembe vyama vya upinzani akimtaka mwenyekiti wa moja ya vyama hivyo ambapo hajataka kuweka wazi ni chama gani akiwataka wanachama wamuulize wapi ziliko pesa.
Polepole kupitia ukurasa wake wa “Twitter” amendika maneno hayo bila kufafanua ni mwenyekiti wa chama gani na hela za nini japo wafuasi wake wengi katika mtandao huo wamechangia mawazo wakitaja huenda ni hela za ruzuku.
Mbali na hilo Polepole pia amesema kuwa kile alichowahi kukitabiri kuwa upinzani hawataweza kushindana na CCM siku za baadaye kimeanza kutimia.
Hii inatafsiriwa kama majibu kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freman Mbowe ambaye hivi karibuni alitangaza chama chake hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika Janurai 2018, endapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitazifanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwezi Novemba mwaka huu.
“Nalipata kuwaambia wataweka mpira kwapani, wakasubiri siku kadhaa na hatimaye imekuwa. Kwa lugha ya shule ya msingi miaka ile ningesema “wameogopa kuputa”, wangeputa waone namna ambavyo kwetu siasa za masuala zinalipa. Ushauri wangu: “Mwenyekiti” lazima aseme hela ziko wapi”, ameandika Polepole.

Comments are closed.