The House of Favourite Newspapers

Drake Amzawadia Babaye Gari la Bentley ‘Siku ya Baba’ 👏🏽

MWANAMUZIKI maarufu wa Marekani, Drake,  juzi aliadhimisha Siku ya Baba Duniani  kwa kumnunulia baba yake, Dennis Graham, gari la pesa mbaya  aina ya Bentley Azure la rangi ya bluu – linalokadiriwa kugharimu Sh.  mil. 340 ($150,000)!

Baba yake huyo ambaye hushiriki kwa kiasi kikubwa kuposti habari mbalimbali za Drake kwenye mitandao, aliandika akimshukuru kwa kumpatia zawadi hiyo yenye thamani kubwa, akijinasibu kuwa ndiye baba mwenye furaha zaidi nchini Marekani katika kuadhimisha Siku ya Baba duniani:

I am the happiest Dad in America for Father’s Day my wonderful Son graced me with a beautiful Bentley for my day Thank You so much my baby boy @champagnepapi it just doesn’t get any better than this, I love it son and I Love you 🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼❤❤❤❤❤

Comments are closed.