The House of Favourite Newspapers

ECOWAS Yafunga Mipaka na Mali

0

VIONGOZI wa Afrika Magharibi wameiwekea Mali vikwazo baada ya serikali ya kijeshi ya nchi hiyo kutangaza kuchelewesha kwa muda mrefu uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao.

Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas, iliyokutana mjini Accra siku ya Jumapili, ilikubali kufunga mipaka na Mali pamoja na kutekeleza vikwazo mbalimbali vya kiuchumi.

Serikali ya kijeshi ya Mali ikijibu ilisema kuwa inafunga mipaka yake ya aridhini na anga na ECOWAS na kuwaita mabalozi wake kutoka nchi wanachama.

Katika taarifa yake, mamlaka ya kijeshi ilisema ililaani ‘vikali’vikwazo “haramu” vilivyowekwa kwa nchi.

Viongozi wa Afrika Magharibi wamekuwa wakitoa wito wa kurejeshwa kwa utawala wa kiraia tangu kundi la maafisa wa jeshi walipompindua Rais Ibrahim Boubacar Keïta kufuatia maandamano ya mitaani mwezi Agosti 2020.

Leave A Reply