The House of Favourite Newspapers

ECOWAS Yawawekea Vikwazo Viongozi wa Mali

0

JUMUIYA ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, Ecowas imeweka vikwazo dhidi ya viongozi wa mpito wa Mali na familia zao, Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku ya kusafiri na kufungia mali zao na fedha.

 

Hatua hii imekuja baada ya kushindwa kwao kuzingatia ratiba ya kurejesha nchi kwenye utawala wa kikatiba ifikapo Februari mwaka ujao.

 

Jumuiya hiyo ilikuwa imeondoa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa nchi hiyo kutokana na mapinduzi ya mwaka jana baada ya jeshi kuahidi mchakato wa mpito wa miezi 18.

 

Taifa la Mali limeshuhudia mapinduzi mara mbili tangu mwaka jana na iko katika mtego wa waasi wenye misimamo mikali.

Leave A Reply