“Muziki mnene mwaka huu utaenda sanjari na Kampeni ya NJE NDANI ambapo vipindi vinne vitarushwa mojakwa moja katika mtaa husika kwa siku ya ijumaa, vipindi hivyo ni Joto la asubuhi, Sports headquarters,uhondo na landha 3600” alisema Ssebo.
Kipindi cha funga mtaa kitakuwa kikirushwa live Siku ya Jumamosi ambayo pamoja na burudani itakayotolewa na RDjs wa efm na kutakuwa na jogging asubuhi, singeli michano, kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki wa singeli,mpira wa miguu Kati ya timu ya efm na timu za maveterans na timu za mikoa husika.
Mbali na hayo pia Ssebo alieleza kuwa kutakuwa na kampeni ya ugawaji mafuta katika mikoa ya Tanga, Mtwara, Pwani na Dar ambapo vyombo vya moto vyenye stika ya masafa ha efm vitapata mafuta hayo bure.
Lengo kuu la Tamasha hilo ni kukutana na kuwashukuru wasikikizaji kwa namna walivyoipokea Efm redio na kushirikiana nao hadi sasa katika maeneo mbalimbali ya jini la Dar na mikoa mingine ambayo hivi sasa efm inasikika ikiwemo pia kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.