The House of Favourite Newspapers

EL CLASICO: VITA YA BARCELONA VS MADRID, HAKUNA MBABE

Mchezo wa pili wa El Clasico kati ya mahasimu Fc Barcelona na Real Madrid kwa msimu wa La Liga wa 2017/2018 uliopigwa katika dimba la Camp Nou usiku wa kuamkia leo ulimalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, ndio alianza kuipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 10, ya mchezo, iliwachukua dakika nne kwa Madrid kusawazisha goli hilo kupitia kwa nyota wake Cristiano Ronaldo.

 

Katika dakika ya 52, mshambuliaji Lionel Messi, aliipatia klabu yake goli la pili baada ya kuihadaa ngome ya ulinzi ya Real Madrid, Nyota toka Wales, Gareth Bale, alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya 72 ya mchezo.

 

Barcelona walicheza pungufu ya mchezaji mmoja katika mchezo huo baada ya Sergi Roberto, kutolewa kwa kadi nyekundu.

Klabu hiyo imendeleza rekodi yake nzuri ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika msimu huu.

Tayari Barcelona, ni mabingwa wa La Liga msimu huu wakiwa na alama 87, na wanasaliwa na michezo mitatu huku Madrid, wakiwa na alama 72 katika nafasi ya tatu na wakisaliwa na michezo miwili kabla ya ligi kumalizika.

Atletico Madrid walioko nafasi ya pili wakiwa na alama 75, wakicheza katika uwanja wao wa Wanda Metropolitano, walikubali kichapo cha magoli 2-0 Espanyol.

 

Katika michezo mingine Las Palmas, walifungwa nyumbani na Getafe, kwa goli 1-0 na Alaves wakawatambia Malaga, kwa kuwachapa kwa magoli 3-0.

BARCELONA (4-3-3): 

Ter Stegen; S. Roberto, Pique, Umtiti, Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta (Paulinho 57); Coutinho (Semedo 46), L. Suarez (Alcacer 90+2), Messi

Subs not used: Cillessen, Vermaelen, D. Suarez, Dembele

Goals: L. Suarez 10, Messi 52

Bookings: L. Suarez 44, Messi 45, Rakitic 86

Red card: S. Roberto 45+3

REAL MADRID (4-3-3): 

Navas; Nacho (Vazquez 68), Varane, Sergio Ramos, Marcelo; Modric, Casemiro, Kroos (Kovacic 84); Bale, Benzema, Ronaldo (Asensio 46)

Subs not used: Casilla, Vallejo, Theo H., Ceballos

Goals: Ronaldo 15, Bale 72

Bookings: Nacho 12, Varane 31, Sergio Ramos 44, Bale 76, Marcelo 77

Referee: Alejandro Hernandez

Comments are closed.