Esha Buhet: Aunt ana roho jamani!

NI ngumu sana kusikia staa akimpigia saluti staa mwenzake lakini kwa msanii wa Bongo Muvi, Esha Buhet ni kama maji tu, kwani ametoa sifa kubwa kwa msanii mwenzake Aunt Ezekiel kwa kuweza kuthubutu kumpa sehemu ya kuuzia chakula chake kwenye pub yake ya The Luxe, iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Esha aliiambia Za Motomoto ya Risasi kuwa siku hizi ni ngumu kuona mwanamke anamuinua mwanamke mwenzake, wengi wamejaa wivu usiokuwa na maana hata kidogo.

“Kwakweli nathubutu kusema kuwa Aunt hana wivu hata kidogo na ana roho nzuri maana kunipa tu nafasi ya kufanya biashara yangu bila kuangalia mimi nitapata au vipi ni moyo wa ajabu sana na namuomba asiache kusaidia na wengine tena,” alisema Esha.

STORI  IMELDA MTEMA


Loading...

Toa comment