The House of Favourite Newspapers

Etihad Yasherehekea Mwaka Mmoja wa Mafanikio Yake Tanzania

1a

????????????????????????????????????

Grace Kijo, Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad nchini Tanzania akigawa chokoleti kwa abiria siku ambayo shirika hilo liliadhimisha mwaka wake wa kwanza wa huduma zake hapa nchini.

Shirika la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake nchi za falme za kiarabu, limetimiza mwaka mmoja wa mafanikio tangu lianze kufanya huduma zake nchini Tanzania ikiwamo kuleta mabadiliko makubwa kwenye biashara ya usafiri wa anga kwa wasafiri wa Dar es Salaam na makao makuu ya falme hizo, Abu Dhabi.

Zaidi ya wasafiri 60,000 wametumia usafiri huo tangu kuzinduliwa kwa huduma zake ambazo zinawaunganisha abiria wengi na miji mikubwa duniani, tangu Desemba Mosi 2015. Wasafiri wengi wamekuwa wakitumia usafiri wa Shirika la ndege la Etihad kutokana na shirika hilo kuwa kitovu cha safari za kwenda Ulaya na Asia.

Shirika hilo linatoa huduma zake kwa kutumia ndege mbili za Airbus A320 yenye nafasi 16 kwa daraja la kwanza na viti 120 kwa daraja la kawaida.

Dar es Salaam ni jiji la tatu kwa Shirika la Ndege la Etihad kutoa huduma katika ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Nairobi-Kenya na Entebbe-Uganda.

Meneja Mkuu wa Kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara wa Shirika la Ndege la Etihad, John Friel alisema, ” Kwa mwaka mmoja tangu kuanza kwa huduma zetu kumekuwa na mafanikio makubwa, ndiyo sababu tuliamua kuichagua Tanzania kwa ajuili ya kufanya shughuli zetu. Tunafurahia kufanya kazi kwa ufanisi jambo ambalo limewavutia wateja wengi kulingana na mahitaji ya soko la usafiri wa anga hapa nchini.”

“Lengo letu ni kuendelea kushirikiana na wadauwa sekta hii ya anga hapa nchini ili kuhakikisha kwamba abiria wengi zaidi wanatumia usafiri wetu ambao umepata heshima kubwa ulimwenguni kwa kunyakua tuzo mbalimbali za ubora zinazotolewa na Shirika la Ndege la Etihad,” alisema.

Shirika la Ndege la Etihad linatoa huduma zake kwenye miji zaidi ya kumi barani Afrika ikiwamo;Johannesburg, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam, Khartoum, Casablanca, Rabat, Lagos, Cairo na Mahé nchini Seychelles.

Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad (EAG) linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika saba mengine ambayo; Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi chini ya Etihad.

Shirika la Etihad lenye makao makuu yake Abu Dhab limejiwekea malengo ya kuhudumia abiria na usafirishaji mizigo maeneo zaidi ya 110 na kutoa huduma bora ya usafirishaji mizigo Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boing 120, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa; ikiwamo 71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s na 10 Airbus A380s.

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Kwa mawasiliano zaidi;

Damian James,

Ofisa mawasiliano wa Shirika la Ndege la Etihad

Baruapepe: [email protected]

Simu: + 9712 511 1035

Comments are closed.