The House of Favourite Newspapers

EWURA Yatangaza Punguzo la Bei ya Mafuta Ambalo Halijawahi Tokea Nchini, Petroli Sh2,994

0

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Jumanne Mei 31, 2022  imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano Julai 1, 2022

 

Bei mpya ya mafuta ya petroli na dizeli nchini imepungua kati ya Sh102 hadi Sh198 kwa lita moja kuanzia kesho Jumatano Juni Mosi 2022 ukilinganisha na ilivyokuwa kwa mwezi uliopita.

 

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo inaonyesha kupungua kwa Sh152 kwa bei ya lita ya petroli hadi kufikia Sh2,994 ukilinganisha na Sh3,148 ya mwezi Mei 2022.

 

Kwa mafuta ya dizeli kwa Mkoa wa Dar es Salaam bei imepungua hadi Sh3,131 kwa lita ukilinganisha na Sh3,258 ya mwezi uliopita sawa na upungufu wa Sh127.

 

Kwa mkoa wa Tanga bei ya lita ya petroli na dizeli imepungua kwa Sh176 na Sh102 hadi kufikia Sh2, 985 na Sh3,162 katika kipindi husika.

Kupungua huku kwa bei za mafuta kunakuja wiki tatu baada ya Raisi Samia Suluhu Hassan alipotoa maelekezo kwa Wizara ya Nishati kushughulikia suala hili na kuonyesha nia ya serikali kuabiliana na ongezeko la bidhaa hiyo inayoathiriwa zaidi na ongezeko katika soko la dunia.

 

 

Leave A Reply