The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: Patoranking Ampa Shavu Msanii wa Bongo – Video

MSANII maarufu wa Nigeria, Patoranking ametua Bongo kwa ajili ya kumtambulisha msanii mpya wa Tanzania, Walid ambaye amemsainisha kwenye Record Lebo yake iitwayo iitwayo Amari Music.

 

Baada ya kutua Bongo, Patoraking alifunguka kuwa alikutana na Walid nchini Holland miaka miwili iliyopita na msanii huyo alipomsikiliza nyimbo zake, Patoraking aliipenda kazi ya kijana huyo na kumuahidi ndani ya miak miwili angemchkua na kumsainisha kwenye lebo yake hiyo mpya.

 

Aidha, Patoraking alisema kwa sasa tayari amefanya nyimbo mbili akishirikiana na Walid ambazo zimeshatoka na kusema msanii huyo ndiye anamuandikia mashairi yake kwa lugha ya kiswahili.

VIDEO: MSIKIE PATORAKING AKIFUNGUKA

Comments are closed.