The House of Favourite Newspapers

FAIZA AKIPATA UKIMWI MAMBO HADHARANI

KAZI kwelikweli! Staa asiyeishiwa vituko kunako Bongo Movies, Faiza Ally, amefunguka kuwa endapo itatokea bahati mbaya akakwaa ugonjwa wa Ukimwi a.k.a ngoma, kamwe hatajificha au kujiona tofauti, bali atajitangaza hadharani na kuwapa watu moyo kuwa wanaweza kuishi miaka mingi zaidi.

 

Akistorisha na Gazeti la Ijumaa, Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili alisema anawashangaa wenye tatizo hilo ambao hujificha na hata wengine kuambukiza wengine, lakini kwa upande wake ataweka hadharani ili kuwapa elimu wengine na kuzuia maambukizi mapya.

 

“Kama mimi ningekuwa na Ukimwi, ningejitangaza hadharani bila woga wowote wala aibu na tena nitasaidia watu wengine wajiepushe na maambuzi mapya,” alisema Faiza.

Comments are closed.