The House of Favourite Newspapers

Faiza Atemea Mate Pesa za Wanaume

MWANAMAMA wa Bongo Movies, Faiza Ally ametemea chini mate pesa za wanaume akisema kuwa hazitamani kwa sababu siku zote, unapozitumia unakuwa hauko huru hivyo ni bora kusaka za kwako mwenyewe ndiyo suluhisho.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Faiza alisema kuwa, ukiwa unatumia pesa ambazo umezitafuta kwa jasho lako, unaweza kujivuna nazo kwani hazina mashariti yoyote.

 

“Tangu nimeamua kutumia pesa ninazozipata kwa jasho langu mwenyewe, nimekuwa na amani na maisha yangu kwa sababu ninaifurahia kwa dhati hivyo pesa za mwanaume nazitemea mate chini,” alisema Faiza.

Comments are closed.